Bill Nas atuhumiwa kuhamisha verse yake kwenye wimbo wa msanii chipukizi na kuiweka kwenye wimbo wa Nuh - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 10 October 2016

Bill Nas atuhumiwa kuhamisha verse yake kwenye wimbo wa msanii chipukizi na kuiweka kwenye wimbo wa Nuh

bill
Rapper Bill Nas anatuhumiwa kutumia verse za wimbo wa msanii chipukizi ambaye amefanya cover ya ‘PanaChris Roby kwenye wimbo wa Nuh Mziwanda.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Bill Nas alitoa verse aliyoweka kwenye wimbo wake na kuhamishia kwenye wimbo wa Nuh Mziwanda.

''Bill Nas alikuwa mshikaji wangu tangu siku nyingi, tulifanya nyimbo wakati akiwa na wimbo wake wa ‘Ligi Ndogo’. Baada ya muda Bill Nas kuona wimbo nachelewesha kuutoa akahamishia verse yake kwenye wimbo wa Nuh Mziwanda ambao bado haujatoka lakini tayari wameshafanya mpaka video,'' amesema Chris.

''Wakati ambao mimi nilikuwa nataka kuuachia wimbo huo nilimpigia simu nahitaji support yake aliniambia nisiuachie kwa kuwa tayari verse kashahamishia kwenye wimbo wa Nuh. Nikaamua kuachana na project hiyo nikaamua kufanya cover ya wimbo huu wa ‘Pana’.”

Akijibu tuhuma hizo Bill Nas ameiambia Jumaa Lunduno kuwa hamfahamu kabisa msanii huyo na wala hajawahi kumsikia. Cover version ya wimbo wa ‘Pana’ ulioimbwa na Chris Roby ni moja kati ya cover kali zilizowahi kuimbwa na baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva.

Cheki hapa video ya  Chris Roby - {Pana Cover Tekno...}


https://cldup.com/Lh-bzXMVlD.mp4?download=PANA%20COVER%20SWAHILI%20-%20BY%20CHRIS%20ROBY.mp4

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here