Diamond Platinumz:- Nimefanya nyimbo 2 na Rich Mavoko muda wowote tunaweza kuziachia - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 4 November 2016

Diamond Platinumz:- Nimefanya nyimbo 2 na Rich Mavoko muda wowote tunaweza kuziachia

Image result for Diamond Platnumz wcb
Member wa WCB au Mkali wa wimbo ''Salome'' na mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya wa Rich Mavoko.

Diamond Platnumz amesema Rich Mavoko ana nyimbo nyingi ndani huku akidai kuna wimbo unaitwa ‘Sijaona’ ambao WCB nzima imekubali lakini yeye anasea bado anaandaa kali zaidi.

''Mimi mwenyewe nimefanya nyimbo nafikiri mbili na Richard na muda wowote zinaweza kutoka,''

Diamond alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
''Sema Richard ni mtu fulani ambaye anajipanga hivyo kipindi hiki anajipanga akianza kufumuka na mabomu yake ni hatari, maana anajipanga kila wimbo akirekodi anakwambia hii bado, akirekodi nyingine tena anakwambia hii bado yaani naweza kusema Richard ni msanii ambaye ana nyimbo nyingi sana kali,''

''Kuna wimbo pale unaitwa ‘Sijaona’ WCB nzima wanaikubali lakini yeye anakwambia hii bado, ila akisema hivyo akileta ngoma nyingine inakuwa kali zaidi. Kwa hiyo ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu kamjalia kipaji na mwenyewe anakuaga hana papara'' Aliongeza

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri kitaifa na kimataifa na wimbo ‘Imebaki Story’.
 Image result for Diamond Platnumz wcb
Rich Mavoko & Diamond Platinumz

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here