
Rapa Mkali anaeiwakilisha A-Town_Arusha Lord Eyes kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kumtaka msanii Chid Benz_Chuma kutopagawa kwani yeye bado ni msanii mkali sana mwenye uwezo wa hali ya juu.
Hivyo anazidi kumuombe kwa Mungu ili aweze kutoka katika mambo ambayo yanamchanganya pia amemkumbusha kuwa anapaswa kumuomba Mungu kwani kila jambo linawezekana.
Lord Eyes alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kuwa Chid Benz_Chuma asisikilize sana maneno ya watu bali azidi kumuomba Mungu amsaidie kwani kila jambo linawezekana katika dunia hii.
''Na Pia namuombea kwa Mungu Chid Benz a.k.a Chuma_ King Kong namwambia nini asipagawe yaani yeye ni MC mkali sana hivyo asipagawe, namwambia asipagawe najua hajapagawa ila asipagawe, siyajui maisha yake kwa sasa lakini ni mwanangu namuombea Mungu kwani sijamuona siku nyingi nina uhakika atakuwa ‘fresh soon as possible’ kwa Mungu kila kitu kinawezekana namkumbusha pia amuombe sana Mungu'' alisema Lord Eyes

Chid Benz a.k.a Chuma
No comments:
Post a Comment