Nikki wa Pili afunguka na kumtaja msanii bora kwake kwa Mwaka 2016 - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 6 November 2016

Nikki wa Pili afunguka na kumtaja msanii bora kwake kwa Mwaka 2016

Image result for Nikki wa Pili fiesta 2016
Mkali wa Hip Hop Nikki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa kwa mtazamo wake kwa mwaka 2016 msanii bora kwake ni Dogo Janja ''Janjaro''.

Kwani msanii huyo ameweza kufaulu kwa kiwango cha juu mtihani ambao unawashinda wasanii, wasomi, wafanyabiashara wengi duniani.

Nikki wa Pili anasema Dogo Janja aliwahi kuteleza na kuanguka lakini ameweza kufanikiwa kuinuka katika kiwango cha juu mno huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu na kuweza kufuta makosa yake.

Pia Nikki aliendelea, na sasa Dogo Janja anafanya show kubwa ambazo zinaacha historia, lakini amekuwa na 'Confidence' iliyovuka mipaka ukilinganisha na umri wake.

''Abduli kachaa A.K.A Dogo Janja kijana mdogo aliyefaulu kwa maksi za juu somo lililowashinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo. ''

''Watu wa rika zote, somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote, show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka, kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016, namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016'' alimalizia Nikki wa Pili
 nikkwapili-20161106-0001
Nikki wa pili & Dogo Janja:

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here