Kama ni mfuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva utagundua kuwa hits nyingi za msanii Nay wa Mitego ni nyimbo ambazo zimetengenezwa na Producer Mr T-Touch.
Wawili ambao wiki chache zilizopita walikua wakifanya kazi pamoja katika studio za Free Nation studio ambayo Nay wa Mitego aliamua kumzawadia producer huyo kwa kile kikubwa ambacho Nay aliamini amefanyiwa na Producer huyo.
Siku chache zilizopita zilizuka taarifa kuwa Mr T-Touch hayupo tena katika studio za Free Nation kwa kile kilichoaminiwa kuwa kuna mifarakano ambayo imetokea baina ya wawili hao. Nay wa Mitego alitafutwa na E.News ya EATV na kuulizwa kuhusu hili na kudai kuwa yeye hana tatizo kabisa na Mr T anakiheshimu kile ambacho amemfanyia..
Leo Clouds E ya Clouds TV imemtafuta Mr T-Touch na kupiga nae story kuhusu issue hiyo na haya ndio yalikua majibu ya Mr T
''Nimeondoka kwa nay kwasababu nataka kuipa thamani kazi yangu, nitafanya kazi na Nay endapo atanilipa nitakavyo. Me nafanya kazi na wasaii wengi na wananilipa pesa nzuri, mfano mzuri Billnass me ananilipa zaidi yaMilioni kwa ngoma moja''
Mr T-Touch aliweka wazi kuhusu kufungua studio yake binafsi na kudai kwamba ametengeneza studio kwa gharama kubwa ila hawezi kupandisha kiwango cha bei ya kurekodi ngoma kwasababu anataka studio yake iweze kufanya kazi hata na ma underground hivyo kiwango ni kile kile cha mwanzo ambacho hata msanii mchanga anaweza kukimudu.
Huu hapa muonekano wa Studio mpya ya Mr T-Touch
No comments:
Post a Comment