Audio: Madee kubadilisha aina ya muziki kisa..? - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 29 August 2016

Audio: Madee kubadilisha aina ya muziki kisa..?


 Image result for madee

Raisi wa Manzese Madee Sheneyda ameamua kubadilisha staili yake ya uimbaji na kubadilika kabisa kwa ajili ya Mtoto wake.

Madee Sheneyda ni moja ya wasanii ambao wamefanikiwa kuwa na mtoto katika Maisha yao ya muziki, mtoto  huyo ambaye anaitwa jina la Saida Madee anayesoma katika shule ya St Frolence darasa la tatu, amekuwa ni chachu ya kubadilisha mwenendo wa muziki wa Madee kwa asilimia kubwa.

Akiongea na 255 Saida Madee anayesoma Darasa la Tatu ameongea kuwa Moja ya kazi ambazo anatamani kuzifanya ni kuwa Nurse, kwasababu anapenda kusoma masomo ya Math, Sayanasi, Kiswahili kwa ajili yakuja kuwasaidia wazazi wake.

Msikilize ''SAIDA'' Mtoto wa madee hapa:

Mbali na hivyo vyote Madee ameamua kubadilisha aina ya ufanyaji muziki wake kutokana na kupata matatizo ambayo yanamfanya mtoto wake kuwa na maswali mengi kwa Baba yake, vilevile matatizo ya Kwenye Media.
  
255 ilimsogozea Kipaza na Madee akawa amefunguka haya

''Kama umegundua sahivi sitaki hivyo vitu na mamabo ya kugombana Gombana na watu kwenye Media, Redio huwa anasikia ananiulizaga flani mbona kafanya hivi flani mbona kaongea hivi'' Alisema Madee.

Msikilize Hapa Madee Sheneyda:

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here