Baada ya Diamond Platnumz kutoa msaada wa Tsh million 20 katika taasisi ya GSM Foundation inayojihusisha na kusaidia watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya vichwa vikubwa na Mgongo wazi sasa ni zamu ya Alikiba.
Msanii huyo wa Bongo Fleva siku ya jana August 11 aliwasili katika ofisi za GSM Foundation na kuwakabidhi pesa taslim shilingi za kitanzania Million 21 (21,000,000) kama mchango wake wa kusaidia upasuaji kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
No comments:
Post a Comment