Baada ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ''Moyo Mashine'' huku video ya wimbo ikiwa inawatazamaji zaidi ya milioni moja, Ben Pol amemtaja Mama yake kuwa ni shabiki mkubwa wa kazi yake.
Moyo Mashine ni ngoma ambayo huwezi acha kuisikiliza pale inapokuwa inakatiza masikioni, hii ni kutokana na mashairi mazuri na sauti nzuri ambayo inafanya ngoma hiyo kuwa pendwa, mbali na Hivyo vyote Ben Paul amemtaja Mama yake kama namba one Fan wake wa ngoma hiyo.
Ben Pol amesema kwamba Mama yake anapenda kazi zake, yaani mama anapenda vocals za mwanae kwa sababu pia anamchango mkubwa kwa kila kazi ambayo anaitoa.
''Mama Ben Pol anapenda sana, Mama Ben Pol anailewa sana Moyo Mashine….Mama anapenda sana kazi zangu hata Chorus nikifanya ananiambia kila kitu,..nadhani Mama anapenda Vocal za Mwanae……………..Familia yangu inanisaidia sana kunishape kimwenendo, kwa mfano labda mama yangu akisikia stori ambayo ipo Negative lazima anipigie…..''Alisema Ben Pol.
Msikilize Ben Pol hapa....
No comments:
Post a Comment