Bill Nas amefunguka kuhusu yeye kuchana kama Godzilla nakusema - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 9 August 2016

Bill Nas amefunguka kuhusu yeye kuchana kama Godzilla nakusema

 
Msanii wa rap nchini,Bill Nas ambaye amekuwa akifananishwa na Godzilla kutokana na style yake ya kuchana amefunguka na kusema kuwa haoni kama style yake ya kuchana inafanana na ile ya Godzilla.

Akihojiwa kwenye kipindi cha The Base cha ITV, Bill Nas amedai kuwa yeye amekuja na muziki wake wa tofauti ambao mwanzo haukwepo kwenye tasnia na yeye haoni kama anamuiga mtu yeyote.

''Mimi nimekuja na style yangu,hata ukiangalia nyimbo zangu zina taste ya tofauti.Sioni sehemu ambapo mimi ninafanana na Godzilla labda kwa vile yeye ana rap na kuimba na mimi nina rap na kuimba hivyo ndio vitu tunafanana''

 Alifunguka ivyo Bill Nas anayetamba na kibao chake cha Chafu Pozi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here