Mwanamuziki kutoka Nigeria ambaye kwasasa amesikika kwenye ngoma ya Perfect Combo, Chidinma amefunguka sababu za muziki wa Nigeria kuwa mkubwa ndani ya Afrika kulinganisha na nyimbo za nchi nyingine nikutokana na kuwa original na sio kuiga muziki kutoka kwenye nchi nyingine.
Chidinma amefunguka hayo baada ya kuhojiwa kwenye kipindi cha The Cruise kinachorushwa na EA Radio mahojiano aliyofanya na King Smash ambapo amesema ''Muziki wa Nigeria umekuwa mkubwa kwakuwa wana sound original, Wamekuwa wao kama wao. Hawa sound kwakukopi muziki mwingine nje ya Nigeria''.
Lakini pia alipoulizwa kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi kati yake na MR Flavor,Chidinma amekanusha nakusema kuwa anamahusiano ya kikazi tu nasio vinginevyo. Pia kuhusiana an skendo zilizosikika siku za nyuma kuwa alishawahi kutoka kimapenzi na Davido na Tekno alikanusha.
Kwa upande wa Bongo kumekuwa na mazoea ya kutengeneza sjendo ili kuweza kutangaza kazi za kimuziki, Kwaupande wake Chidinma amekanusha kutengeneza skendo yoyote ili aweze kukuza kazi zake za kimuziki bali kufanya kazi nzuri tu.
Lakini ameongezea kuwa baada ya kufanya kazi na Joh Makini, Chidinma amesema anatamani kufanya kazi nyingi zaidi na wasanii wengine ikiwemo wa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment