Darassa aelezea changamoto za maisha magumu aliyopitia zinavyomfanya akaze kwenye muziki…
Rapper Darassa ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Too Much
amesema kuwa changamoto za maisha magumu aliyoyapitia ndiyo yanampa
hamasa ya kukomaa kwenye muziki ili aweze kuwa juu zaidi.
Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz kwa Ngaz kinachoruka kupitia
EATV,rapper huyo amedai kuwa amewahi kupitia changamoto nyingi kwenye
maisha ikiwemo kulala njaa na kukosa mahali pa kukaa.
''Changamoto zina njia mbili
zinaweza kukuua kabisa au zikakufanya kuwa bora zaidi, lakini siku zote
mtu mwenye malengo changamoto haziwezi kumuua bali zinamfanya kuwa bora
zaidi. Kazi yoyote nzuri ambayo saizi inafanya vizuri ni kutokana na
changamoto ambazo nimepitia nyuma, kama kulala njaa nyumbani, ama kukosa
sehemu ya kulala au kukosa kitu cha kuvaa na chochote kile ndiyo
kimenijenga mimi kuwa mtu bora ambaye ninajua nini cha kusema, nini cha
kufanya na wapi kwa kwenda'' alisema Darassa.
No comments:
Post a Comment