Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini Dully Sykes ambaye ametoa wimbo wake mpya hivi karibunu ambao unaitwa Inde na kumshirikisha msanii Harmonize ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kujiunga na lebo ya WCB ambayo iko chini ya Diamond.
Dully Sykes ambaye wimbo wake huo ulifanyika kwenye studio za wasafi na gharama zote za video kugharamiwa na lebo hiyo amesema yeye yuko kwenye studio hizo kama kaka tu,na walichofanya WCB ni kama kulipa fadhila kwa kaka yao.
''WCB, mimi ni nyumbani,sijasaini mkataba na wala hatuna hizo plan,mimi nipo hapa kama kaka.Na mimi ndio mtu wa kwanza kumkimbiza Diamond kufungua studio kwa hiyo nafurahi alifanya hivyo pia napenda producer wa hapa,ndio wa maana nimeamua kufanya kazi hapa na wao wamegharamia kila kitu kama kulipa fadhila'' Alifunguka Dully Sykes.
No comments:
Post a Comment