Fiesta ndo kitu ambacho kina trend kila kona saa hii. Na wote tumekwisha jua kuwa Wasukuma ndo kabila la kwanza kula shavu la Burudani isiyo na mfano kwenye Tamasha hilo.
Nikiwa namaanisha kuwa Mwanza ndo utakuwa mkoa wa kwanza kuahirisha usingizi wa wapenda Burudani kwa masaa kadhaa na kukidhi kiu yao ya Burudani ambayo imedumu kwa zaidi ya miezi 23 sasa..
255 ya clouds fm imemtafuta FID Q na kupiga nae story kuwa tamasha la Fiesta kuanzia katika mkoa wake inamuonyesha picha gani! Na hili ndo lilikuwa jibu
''Fiesta kuanzia Mwanza nafkiri ni heshima kubwa sana kwa wana Mwanza na ni baraka pia, lakini pia ni thamani kubwa ambayo wanapewa wana Mwanza kutokana na waandaaji wa tamasha hilo kuiona sapoti ya watu wa Mwanza kwasababu mara nyingi watu wa Mwanza huwa hawawaangushi. Nafikiri utamaduni huu ndio unapelekea hata waandaaji wa Fiesta kuona kwamba kuna umuhimu wa kuanzia Mwanza.''
FID Q alithrowback na sisi kutukumbusha ilikuwa vipi siku anakinukisha katika tamasha la Fiesta kwa mara ya kwanza katika mkoa huo. Na akadai kuwa ni kipindi anasumbua mtaani na ngoma yake ya FIDQ.Com ambapo ilimlazimu kusimamisha show baada ya wana mwanza kuonyesha kuwa wanakoma na flow zake akiwa kwa stage kiasi kwamba wakashindwa kuizuia miili yao kuruka na midundo ya msukuma mwenzao kitu ambacho kilikuwa ni kosa kufuatana na sheria za askari waliokuwa wakisimamia usalama pande hizo.
Unaweza kumsikiliza hapa FID Q anavyofunguka ilivyokua siku iyo ya show.
No comments:
Post a Comment