Rapper Rabbit King Kaka wa Kenya, amewatupia lawama mapromota wa nchini humo kwa kuwalipa fedha nyingi wasanii wa nje kwenye show na kuwapa kiduchu wasanii wa ndani.
Ametoa malalamiko hayo kwenye mtandao wa Facebook na kuwatolea mfano Diamond na Alikiba ambao wamekuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi kila wakitumbuiza nchini humo.
''Sazile Alikiba anakam na analipwa hiyo 2million sio mbaya, Diamond anakam analipwa hiyo 2 Million, Na Nani pia anakam analipwa 2 Million, na Nani pia 2 million but on the same performance utaona wameweka legends wa hapa Kenya na trust me wamepewa 300k, 400k ata unaweza Pata mi 100k (shame, what a shame) sahizo bado yule amekupa show anataka cut yake which sio mbaya but what do fans expect. Hii kitu yote iko connected,'' aliandika Rabbit.
Amedai kuwa wasanii wa Kenya hawapewi heshima wanayostahili na hivyo kudidimiza muziki wa nchi hiyo.
Soma post yake nzima hapa:
No comments:
Post a Comment