Wawili hao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake baada ya kudaiwa kuhitilafiana kwenye masuwala ya pesa.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema yeye hajagombana na Mr Ttouch kama baadhi ya watu wanavyosema.
''Mimi kwangu namchukulia Mr T kama mtoto aliyekuwa nyumbani na sasa amekuwa mtu mzima anaamua kutafuta maisha yake, kwa hiyo mimi namtakia mafanikio mema katika maisha yake,'' alisema Nay.
''Mimi ndiye niliyemtafuta Mr T na kuamua kumkabidhi studio, nikawa sichukui hata shilingi mia, kwa hiyo mimi nachoweza kusema muache aende kwa sababu amekuwa mtu mzima'' aliongeza.
Pia rapper huyo amesema kwa sasa kama ana kazi atamtafuta mtayarishi huyo kwa ajili ya kazi lakini hawezi tena kufanya naye kazi kishkaji kama zamani.
No comments:
Post a Comment