Peter Msechu afunguka kuhusu ujumbe wa tuhuma wa AT - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 15 August 2016

Peter Msechu afunguka kuhusu ujumbe wa tuhuma wa AT



Peter Msechu amefunguka juu ya tuhuma za msanii mwenzake AT aliyedai kumzungumzia juu ya wembamba wake.

Amedai kuwa kwa mtazamo wake hajui nani amemlisha sumu msanii mwenzake huyo lakini ameona ujumbe huo unaodai kuwa anapofanya interview amekuwa akimzungumzia kitu ambacho ni uongo.

''Mara nyingi napofanya interview nimekuwa nikiulizwa kuhusu unene wangu lakini nitakapotolea mfano wa mtu yeyote ambaye ni mwembamba kwenye muziki si mbaya,'' alisema Peter Msechu 

Hata hivyo Peter Msechu amedai kuwa hajawahi kumtaja AT kwenye interview yake yoyote na wala hajawahi kuwa na urafiki na msanii huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here