Katika harakati za kuikamilisha project yake mpya msanii Q Chillah amesema amekwamishwa na dau
alilotajiwa na Jokate ili kutokea kwa mrembo huyo kama vieo queen katika video yake.
Ni video ya “Sungura” ambayo msanii Q Chief alimtaka mwanadada Jokate kutokea kama video queen katika chupa hilo. Lakini mkongwe huyo ameweka wazi kwamba dau alilotajiwa na mrembo huyo limekatisha ndoto zake kwakuwa ni mtonyo mrefu sana tofauti na alivyotegemea.
Q Chief ameweka wazi kuwa sababu za yeye kumtaka Jokate kutokea katika video hiyo ni kutokana na kwamba amemtaja kwenye nyimbo hiyo ya “Sungura”, kwahiyo ingeleta maana zaidi kama muhusika angetokea.
''Sikutegemea kama Jokate angenitajia kiasi chote kile cha pesa, kwasababu tukiangalia pesa ambayo ameitaja na kazi ambayo tunaenda kuifanya video itakuwa inagharimu pesa nyingi sana. Labda tunaweza kumtumia kwa wakati mwingine, lakini tumempa comliment kwenye wimbo, kwasababu tumemtaja na tunamuheshimu.'' Alisema Q Chillah.
No comments:
Post a Comment