Msanii wa muziki wa Singeli, Sholo Mwamba amedai muda si mrefu atakuja na collabo zake na mastaa kadhaa wa muziki wa Bongo Fleva.
Muimbaji huyo amepata umaarufu zaidi baada ya kushirikishwa na Professor Jay kwenye wimbo ‘Kazi Kazi’.
Mfalme huyo wa Singeli amekiambia kipindi cha My Playlist cha Clouds TV kuwa tayari wameshamaliza maongezi na Pam Dee pamoja na Baba Levo na sasa kinachosubiriwa ni kufanya collabo.
Aidha ameongeza kuwa mashabiki wake wakae tayari kwani kuna vingi vizuri vinakuja kutoka kwake ukiwemo wimbo ambao atafanya collabo na Bill Nass na mwingine na Diamond.
Wakati huo huo, amefafanua kuwa hana ugomvi na msanii mwenzake Man Fongo kwa kuwa yeye ndio aliyemfundisha kazi wakati huo akiwa kama Dj wake kwahiyo hachukii mafanikio anayoendelea kuyapata kwenye muziki huo.
No comments:
Post a Comment