SINGELI imeanza ma-bifu kama ya Bongo Fleva -: Msaga Sumu - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday 7 August 2016

SINGELI imeanza ma-bifu kama ya Bongo Fleva -: Msaga Sumu

 
Singeli ni muziki ambao unakuja kwa kasi sana katika tasnia ya burudani nchini Tanzania, wataalamu wa mambo wamesha tabiri kuwa muziki huo utakuja kufanya vizuri sana katika sekta za burudani na kuitangaza vizuri nchi yetu kwasababu sisi ndio waanzilishi wa muziki huo ila endapo tu utawekewa misingi imara.

Tumekuwa tukisikia fununu mitaani kuwa kati ya wasanii wawili wanaofanya vizuri katika muziki huo kuna bifu zito linaloendelea.

255 ya Clouds Fm ikaona sio kesi ngoja imtafute Msaga Sumu hit maker wa ngoma ya “Unanitega Shemeji” ambaye kwa mujibu wake anadai yeye ndiye muanzilishi wa muziki huu, na haya ndio yalikuwa majibu yake.
   
''Kuna kila sababu ya kusema kuwa Singeli nayo inaanza kuleta bifu kwasababu mimi nimeanza muziki huu kabla nyie hamjaujua bado, na siku zote kwenye riziki hapakosi fitina. Mtu anaweza kuwa hapendi kukuona unafanikiwa katika maisha yako.''

255 ya Clouds Fm ikaona isiwe deni, ngoja imtafute na sukari ya warembo kwasasa, hit maker wa ngoma ya ''Hainaga Ushemeji'' Man Fongo naye akasogezewa kitonge na hivi ndivyo alivyo piga story na sisi.

''Hakuna kitu kama hicho, itakuwa haileti maana kama tunaanza kulitengeneza bifu kwa sasa hivi kipindi ambacho muziki wa SINGELI bado unaonekana wa kihuni, bado hatuja utangaza vizuri muziki wetu, inabodi kwanza tupambane tuhakikishe muziki wetu unafika mbali hata kimataifa hapo hata tukitengeneza bifu itakuwa inaleta maana.''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here