Timbulo afunguka haya jinsi Linah na Malaika walivyo mtosa kufanya naye kazi - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Saturday, 27 August 2016

demo-image

Timbulo afunguka haya jinsi Linah na Malaika walivyo mtosa kufanya naye kazi

Responsive Ads Here
.com/blogger_img_proxy/ 
Msanii wa Bongo Fleva Timbulo amesema wimbo wake wa ‘Ngomani’ baada ya kugonga ukuta kwa wasanii wawili wa kike kufanya naye wimbo wake kuanzia msanii Linah na Malaika kutokana na sababu mbalimbali Nay Lee ndiye alikubali bila tatizo.
 .com/blogger_img_proxy/
 Malaika:

Akizungumza na EATV Timbulo amesema baada ya ‘management’ yake na Malaika kukubali kuingiza sauti ya wimbo na kushindwa kutokea kwenye video, Timbulo aliamua kufuta sauti ya Malaika katika wimbo huo na kuingiza ya Nay Lee na kufanya naye kazi hiyo.
 13328952_1031170946958748_1876088491_n
Linah Sanga: 

''Malaika alishindwa kutokea kwenye video kwa sababu vitu alivyokuwa anavitaka ikiwemo mavazi mapya na fedha nilimwambia kazi hiyo tunakwenda kufanyia vijijini hivyo hakuna haja ya mavazi mapya akagoma kutokea ikabidi nimtafute Nay Lee ambaye alikubali bila tatizo lolote'' Amesema Timbulo.

Aidha Timbulo amesema pamoja na kuachia ngoma hiyo bado anaendelea kuwaomba mashabiki waendelee kumuunga mkono katika kazi zake na ataendelea kufanya vitu vizuri zaidi.

Post Bottom Ad