Young Killer ametaja ngoma ya Hip Hop anayoikubali zaidi,soma hapa kufahamu.. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 9 August 2016

Young Killer ametaja ngoma ya Hip Hop anayoikubali zaidi,soma hapa kufahamu..

 
Msanii wa hip hop Tanzania,Young Killer amefunguka na kusema kuwa moja ya ngoma za hip hop anazozikubali duniani ni ngoma ya marehemu Langa inayoitwa Rafiki wa kweli.

Young Killer aliyasema hayo kwenye mahojiano yake na Jabir Salehe kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM akitoa maoni yake juu ya uwezo wa Langa,mwana Hip hop ambaye alifariki miaka miwili iliyopita.

''Langa ni moja ya watu ambao wamefanya ngoma ambazo ziko kwenye Top 3 ya ngoma zangu za muda wote duniani,kuna ngoma yake inaitwa rafiki wa kweli,nadhani ndio ngoma inayojirudia zaidi kwenye playlist yangu,kama angekuwa hai ningefanya naye kazi nyingi sana''

 Alifunguka Young Killer ambaye alidai hamsifii kwa vile amekufa lakini ndio ukweli halisi.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here