Minong’ono inadai kuwa Zari hakubaliki ukweni kutokana na kupenda maisha ya kizungu, kutawala mipango ya Diamond na huenda ndio chanzo cha Bi Sandra kuondoka Madale, nyumbani kwa staa huyo.
Pamoja na Zari kutokubalika ukweli, Diamond haoneshi kushtushwa na hali hiyo kwakuwa hivi karibuni alimzawadia nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 396 ya Afrika Kusini pamoja na kumpeleka visiwani Zanzibar kusherehekea birthday yake.
Labda ndugu za Diamond inabidi waukubali tu ukweli mchungu kuwa Zari sasa ndio kila kitu kwa staa huyo. Wakiwa na mtoto mmoja sasa, Tiffah, wawili hao wanatarajia kuongeza mtoto wa pili December mwaka huu.ama wa msanii wa Bongo flava, Naseeb ‘Diamond’ Abdul, amemtakia heri ya kuzaliwa EX wa Mwanae Wema Sepetu.
Sasa basiii.. ujumbe wa Pongezi wa Mama Diamond umezua minong’ono kwa baadhi ya watu kuwa huenda kuna tatizo kati yake na Mpenzi wa Diamond wa sasa Zari kwa kuwa hakumtakia Heri ya kuzaliwa kwenye siku yake hivi majuzi.
''Happy birthday.. Mamy akee @wemasepetu
mungu akuongezee umri na akujali kheri akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Amin ,” ameandika Bi. Kendrah Jumatano hii.'' Ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram Bibi Tiffah.
Kwa post hiyo inadhihirisha kuwa mambo si shwari kati ya Zari na Mkwewe huyo.
No comments:
Post a Comment