Belle 9: Siwezi kufanya Singeli, ni bubble gum music - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday 13 October 2016

Belle 9: Siwezi kufanya Singeli, ni bubble gum music

Image result for belle 9 2016
Belle 9 amesema hafikirii kabisa kufanya muziki wa Singeli. Muimbaji huyo wa R&B amesema huo ni muziki wa kupita na katu hauwezi kudumu.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM, Prince Ramalove iwapo atafanya muziki huo mashabiki wakimtaka.

''Sitegemei,'' alisema Belle.

''Hata kama nitafanya, sitofanya kama release song sababu Singeli ni muziki fulani hivi ambao unapita, ni bubble gum music. Sasa hivi watu wanaushabikia lakini itafika time utapita, sio muziki wa kustick.''

Msikilize kwenye video hiyo apo utamsikia Belle 9 akizungumzia suala hili kuanzia dakika ya 2:00.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here