Young killer na Dogo janja wamepigana vijembe huku kila mmoja akijitamba kuwa yeye ni mkubwa kuliko mwenzake.
Kupitia eNEWZ, ilimtafuta Dogo Janja na kuzungumza naye na alisema kuwa hajaona msanii wa kushindana nae kwa sababu yeye ndiye ‘role model’ wa madogo wote walioimba muziki hata Young Killer yeye ndiye aliyemshawishi aingie kwenye muziki kwa hiyo ''huwezi fananisha Port na Bugati''
Young Killer mimi ndiyo niliyemuinspire kenye muziki kwa hiyo muache aongee tu, kingine huwezi fananisha port na bugati.'' amesema Dogo Janja.
Pia eNewz ilimtafuta Young Killer na kuzungumza naye, alisema kuwa haoni kama dogo janja anaimba rap bali anaimba miziki yao ya kibiashara na yeye ngoma yake ya mwisho aliyofanya na Mr. Blue ndiyo aliyofanya rap kweli. Pia aliongezea kwa kusema kuwa yeye ndiyo mkali kuliko wote.
Hata hivyo sisi tumewaachia mashabiki waseme wanaonaje kwa mtazamo wao kuhusu mtanange huo.
No comments:
Post a Comment