Galatone afunguka na kuweka wazi inshu ya kwenda kwa mganga ili kufanya makeke - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 28 October 2016

Galatone afunguka na kuweka wazi inshu ya kwenda kwa mganga ili kufanya makeke

 Image result for Galatone - samaki
Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘SamakiGalatone amefunguka na kusema kuwa yeye aliwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji kufanya makeke ili aone jambo ambalo linamsumbua.

Galatone alisema hayo kupitia kipindi cha
NgazKwaNgaz’ kinachorushwa EATV, msanii huyo anasema katika hali ya kawaida kuna mambo yanaweza kukutokea na kukufanya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kujua tatizo.
  
''Yah kwa mganga mimi nimeshawahi kwenda, unajua katika maisha ya kila siku tunayoishi kibinadamu kuna vitu vingine vinaweza kukutokea ukahisi hiki kitu ni cha tofauti na si cha kawaida.

Aliongeza ''Kwa mfano umelala vizuri msafi halafu unaamka asubuhi unajikuta una matope mwili mzima hivyo hicho hakikufanyi uende kwa mganga kweli? Kitu hiki kinaweza kukufanya ukaingia kwenye imani ukawaambia jamanii eehh niangalizieni hiki kitu” alisema Galatone

Mbali na hilo Galatone anasema kipindi anasoma anakumbuka maisha yalikuwa taiti na pesa anazopewa zilikuwa hazitoshi kwa matumizi yake hivyo alikuwa mwizi sana wa vitu vya watu kiasi cha wanafunzi wote hostel walikuwa wanajua kuwa jamaa ni mpigaji kwa vitu vya shule kama Blue band, misosi n.k.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here