Ukimya umetawala juu ya suala hilo, ndio sababu zilizofanya Perfect255 kupiga story na mkali huyo na kutaka kujua uliishia wapi mchongo huo.
''Project ya wanandoto remix inaenda vizuri na washiriki wote 8 wamekwisha ingiza sauti, kutoka mikoa mbali mbali na mmoja kutoka Kenya. Imebaki tu sehemu yangu mimi kwasababu nina kama miezi miwili sipo Dar, niko mikoani kuna kazi fulani naifanya na hivyo mimi ndio nimekuwa kama kikwazo katika ucheleweshwaji wa hii project. Lakini all & all mwishoni mwa mwezi wa 11 narudi Dar es Salaam na kitu cha kwanza ni kwenda studio na kukamilisha hicho kitu na baada ya hapo process zingine zitafuata.''
Hayo ndio yalikuwa majibu ya Kala Jeremiah kipindi akipiga story na Perfect255.
No comments:
Post a Comment