Izzo Bizness asema hakuna kitacholiyumbisha Kundi la ‘The Amazing’ - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 21 October 2016

Izzo Bizness asema hakuna kitacholiyumbisha Kundi la ‘The Amazing’

 Image result for izzo bizness na Abela
Mmoja kati ya wasanii wanaounda Kundi la The Amazing Izzo Bizness amesema kundi hilo limejipanga kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiyakabili baadhi ya makundi ya muziki.

Rapper huyo ambaye ameshirikiana na mwanadada, Abela kuunda kundi hilo "The Amazing" Izzo Bizness ameiambia Jumaa Lunduno.blogspot.com kuwa kabla ya kuunda kundi hilo walikaa chini na kuangalia namna ambavyo wataweza kukabiliana na matatizo.

''Sisi tumejipanga kupambana na changamoto zote, mpaka kuja au kufikia maamuzi ya kuungana na kuanzisha kundi tayari tumeshasomana tabia, yaani sisi tuna mengi ambayo tuliyaangalia. Kwahiyo naweza sema tupo vizuri tunaomba Mungu atusimamie tu,''

Pia rapa Izzo Bizness amesema muziki kwa sasa umebadilika na kuwafanya wasanii kuacha kutegemea show pekee.

''Kwa sasa ukifanya muziki mzuri utaona matunda ya muziki wako kwa sababu sasa hivi wasanii hatutegemei shows tu, watu wanapata deal kubwa za kupiga show za mkampuni, endorsement na mambo mengine. Kwahiyo mimi naona kuna mashavu mengi sana kwenye muziki kama ukiandaa kazi nzuri,'' alisema Izzo Bizness.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here