Mkali wa nyimbo za harakati na aliyekuwa
mgombea wa Ubunge kupita tiketi ya Chama cha ACT, Kalama Masoud, ‘Kalapina’
Pia anafahamika kama mmoja wa wasanii wakorofi sana na sasa amegeuka kuwa mkombozi wa vijana na wasanii wenzake walioathiriwa na matumizi ya Dawa za kulevya.
Kalapina alikuwa pia akifahamika kwa style yake yakuziba jicho moja ambayo siku hizi haonekani nayo tena.
Kupitia Planetbongo Pina amesema kutoonekana akiziba jicho moja kama zamani ni sawa na mtu kubadili mtindo wake wa nywele kwa hivyo si jambo la ajabu siku tukimuona kairudia tena.
Kutokana na harakati zake hizo, alikuwa mmoja wa waliochangia sana Chidbenz kwenda kupata matibabu ya kuachana na Unga kule bagamoyo.
Amewatoa shaka mashabiki wake kuwa harakati anazofanya kwasasa bado hazimzuii kufanya muziki kwani tayari ana ngoma yake inaitwa “Asiyehusika na show”.
Hilo jina la wimbo linafanana na kauli iliyosikika kwenye video moja iliyosambaa mitandaoni miaka ya nyuma ikimonesha kalapina akimtaka Chidbenz ashuke jukwaani baada ya kuingilia show yake. alisika akisema “Asiyehusika na show ashuke”.
No comments:
Post a Comment