KR Muller ambaye kwa sasa ni member wa Rada Entertainment anajipanga kumtafuta kiongozi wa TMK Wanaume Halisi, Juma Nature ili kumaliza tofauti zao.
Juma Nature amekuwa akimtuhumu KR kuaribikiwa baada ya kuhama TMK na kuhamia Rada Entertainment ya TID.
Akiongea na Bongo5 wiki, KR amesema anajipanga kumtafuta Juma Nature ili kuzungumzia yaliyotokea.
''Kusema kweli haya mambo yameniharibia sana, kuna wakati wazazi wangu baada ya kusikia nimeokotwa nikiwa nimelewa chakari walijisikia vibaya sana,'' alisema KR. ''Sijaonana na Juma Nature kwa muda mrefu, lakini napanga kumtafuta ili tuzungumze kwa sababu sisi tumetoka mbali,''
Rapa huyo amesema kwa sasa anafurahia maisha mapya ndani ya label ya TID, Rada Entertainmet.
No comments:
Post a Comment