Weekend iliyopita Fiesta ilikuwa pande za Arusha. Kitu ambacho kilimake headlines pande hizo ni baada ya mmoja wa kundi la Weusi ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu (Lord Eyes) kupanda jukwaani na msanii Baraka Da Prince wakati kundi lake la Weusi nalo lilikuwa na show usiku huo.
Kitu ambacho kilizua maswali mengi kwa wapenzi wa muziki wa Hiphop haswa wale ambao walikuwa wamemiss uwepo wa Lord Eyes kwenye game ya music na kuzua sintofahamu kuwa Lord huenda ameondoka katika kundi la Weusi au la!
Leo kwenye kipindi cha XXL Lord Eyes alikuwa mgeni na kuweza kupiga story kadhaa na watangazaji wa kipindi hicho. Na moja kati ya maswali ambayo aliulizwa mkali huyo ni pamoja na ''Ni kwanini hakuperform na kundi la Weusi usiku ule''.
''Nilipanda na Baraka Da Prince kwasababu Baraka ndiye aliyeona umuhimu wangu mimi kuwepo Arusha. Alinifata nikiwa bado sijapokea simu ya mtu yeyote.''
Na hicho ndicho alichokisema Lord Eyes.
No comments:
Post a Comment