Maneno ya Abby Skills haya kuhusu yeye na madawa, pia atoa shukrani hizi kwa Alikiba pamoja na Mr Blue - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 31 October 2016

Maneno ya Abby Skills haya kuhusu yeye na madawa, pia atoa shukrani hizi kwa Alikiba pamoja na Mr Blue


Msanii wa Bongo Fleva Abby Skills amesema anawashukuru sana wasanii Ali Kiba pamoja na Mr. Blue kwa kumrejesha kwenye game la muziki baada ya kupotea kwa miaka minne mfulilizo.

Abby Skills ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV ambapo pia alitambulisha ngoma yake mpya na video yake inayokwenda kwa jina la 'Averina' ngoma ambayo amewashirikisha Ali Kiba pamoja na Mr. Blue.

''Ninawashukuru sana Ali Kiba pamoja na Mr. Blue kwa kunirudisha kwenye game , ni watu ambao tumekuwa pamoja na wameisapoti sana kazi yangu hii.'' Alifunguka Abby Skills

Kwa upande wake Mr. Blue amesema Abby Skills ni mtu muhimu sana katika maisha yao ya muziki hivyo wapo naye na watazidi kushirikiana naye katika mambo mbalimbali. 

Pamoja na hayo Abby Skills amesema pamoja na kuwa nje ya game kwa muda wote lakini hajawahi kukata tamaa na kujiingiza kwenye vitendo vya madawa ya kulevya kama ilivyo kwa wasanii wengine na kusisitiza kwamba ataendelea kupambana ili kuhakikisha anarejea kwenye game kama zamani na kuwataka mashabiki kumuunga mkono kwa kazi anazofanya. 
 official_abbyskillz-20161029-0001
Mr Blue, Abby Skills & AliKiba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here