Msanii Mkongwe katika mziki wa Bongo Fleva nchini Mr. Blue ameweka wazi kwamba pamoja na kukubalika na mashabiki wengi na kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu hajawahi kupata tuzo hata moja ya kutambua mchango wake kwenye muziki.
Mr. Blue Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV, Blue amesema anatambua umuhimu wa msanii kupata tuzo ila kwa bahati mbaya yeye hajawahi kupata tuzo yoyote.
''Mimi sijawahi kupata tuzo yoyote siyo ya kitaifa wala ya kimataifa ila ninachoamini mimi ni kwamba mimi ni ‘expensive’ na ndiyo maana natoa ngoma mara moja kwa mwaka na inadumu kwa muda mrefu'' Alifunguka ivyo Mr. Blue
Aidha Mr. Blue ameongeza kuwa tuzo ambazo
zimeanzishwa na kituo hicho za EATV AWARDS zitasaidia sana wasanii wengi kuweza kutambulika zaidi na anaamini pengine anaweza kupata tuzo hiyo na ikawa tuzo yake ya mara ya kwanza.
No comments:
Post a Comment