Msaga Sumu ambaye amejitambulisha katika game kupitia muziki wa singeli ametoa ufafanuzi huo wakati akiitambulisha rasmi video ya wimbo huo, kupitia kipindi cha FNL, cha EATV, na kuongeza kuwa huo ni ujumbe kwa watu wote ambao wamekuwa na kawaida ya “kukopi” vitu vya watu bila kuumiza vichwa wala kutambua kazi ya muanzilishi.
Akizungumzia video hiyo, Msaga Sumu amesema ameamua kuwa serious katika muziki na ndiyo maana amefanya kitu kikubwa zaidi katika video hiyo ambayo ameonesha mazingira halisi ya uswahilini.
Kuhusu yeye kufunikwa na baadhi ya wasanii wa singeli walioshika chati hivi sasa, Msaga Sumu ameendelea kusisitiza kuwa yeye ndiye baba wa muziki wa singeli na hakuna mtu atakayeweza kumfunika.
No comments:
Post a Comment