Msanii Motra the Future ashangazwa na P-funk kuachia wimbo wake Mpya bila kujua - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday 20 October 2016

Msanii Motra the Future ashangazwa na P-funk kuachia wimbo wake Mpya bila kujua

Image result for Motra the future
Msanii anayefanya poa kwenye mziki wa Hip Hop kutoka Arusha, pia anafanya vizuri kwa sasa na ngoma zake pamoja ya One Day ambayo ndani amemshilikisha mwanadada Ruby na Cover alizofanya, Motra the Future, kashangazwa na kitendo cha P-funk kuachia kazi yake.

Kinachoonekana Motra the future hakujua kabisa kuwa wimbo wake ft Baraka Da price upo mtandaoni na mtu yeyote anaweza kuusikiliza katika website ya Bbc.

Project ya Motra the future aliyofanya kwa P-funk huenda ilitegemewa kutoka kwa style ya kipekee hasa kutokana na tetesi za motra kumkimbia producer wake Mona Gangstar na kukimbilia kwa P-funk jambo ambalo baadaye walilikanusha.

Kupitia Planet Bongo ya EA radio, Motra the future aliulizwa endapo ana taarifa hizo akashtuka na kuhoji kwanini P-funk ameamua kuutoa wimbo huo wote bila kumshirikisha?

Motra amesema alikuwa akijipanga kwenda kuuchukua ili kuuachia rasmi lakini hakujua tayari upo mtandaoni.

Wimbo huo unasikika kwenye site ya Bbc katika makala maalumu kuhusu muziki wa Bongo fleva iliyoandaliwa na mtangazaji wa shirika hilo Salim Kikeke.

Katika makala hayo kwa lugha ya kiingereza P-funk anasikika akielezea jinsi ya kutengeneza Beat na mwisho wimbo wa Motra ft baraka unasikika wote.

Taarifa za uhakika zinaeleza tayari motra ameshaondoka kwa monagangstar na ana management mpya itayosimamia kazi zake.
Image result for p funk majani


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here