ROMA azipangua skendo za kuwa na Watoto nje ya ndoa - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 18 October 2016

ROMA azipangua skendo za kuwa na Watoto nje ya ndoa

Image result for roma mkatoliki
Msanii Roma Mkatoliki amempa zawadi ya wimbo mtoto wake anayeitwa Ivan katika siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka minne, lakini kuna tetesi kuwa rapa huyo ana mtoto mwingine nje ya ndoa.

Ukiongelea wasanii ambao wanafanya vizuri kwa upande wa hip hop huwezi kuacha jina la Roma Mkatoliki.

eNewz ilipiga story na Roma na alisema kuwa hizo skendo hazikuanza leo kwa sababu tayari aliwahi kupata skendo ya yeye na aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha TV cha Nirvana, Lotus Kyamba kuwa mtoto aliyenaye ni wa kwake licha ya kwamba siyo kweli na kwamba yeye ana mtoto mmoja pekee ambaye ni Ivan.
 roma2030-20161018-0003
 Roma na Ivan 

"Mimi kiukweli nina mtoto mmoja tu wa kiume ambaye ni Ivan na hizo story za mimi kuwa na mtoto nje zipo niliwahi kuambiwa nina mtoto na lotus kumbe siyo kweli na huwa sipendi kuziongelea sana kwa sababu mimi nina mke wangu na nina mtoto mmoja tu ambaye ni Ivan"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here