Soggy Doggy: ‘Siwezi kuimba wala kufanya singeli’, Bado nipo kwenye ‘game’ la Hip Hop - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 22 October 2016

Soggy Doggy: ‘Siwezi kuimba wala kufanya singeli’, Bado nipo kwenye ‘game’ la Hip Hop

 Image result for soggy doggy hunter
Mkongwe katika game la hip hop ambaye amewahi kuishika game ya bongo fleva miaka ya nyuma, Soggy Doggy Hunter, amesema hajaacha muziki, licha ya kutosikika akitoa kazi mpya kwa kipindi kirefu.

Soggy amewatoa shaka wapenzi wa bongo fleva, alipokuwa akizungumza na EATV, ambapo amedai kuwa kila siku anaandika ngoma mpya na kwamba hadi sasa ana ngoma zaidi ya 16 alizokwisha rekodi, lakini hajaziachia kwa kuwa bado anausoma mchezo.

''Siwezo kuacha muziki bro, hapa nilipo ni kama ngoma 16 hivi, zipo tu, utazisikia muda si mrefu'' amesema Soggy Doggy.

Kuhusu uwezekano kubadili aina ya muziki ili kuendana na soko, Soggy amesema kuwa anaendelea na mtindo ule ule kwa kuwa yeye ni mwana hip hop.

''Siwezi kuimba wala kufanya singeli, naendelea na hip hop kama kawaida'' Amesema Soggy
Soggy amewahi kutamba na ngoma kama vile ‘Kibanda cha simu’ na ‘Nilikaona mwaka jana’ kabla ya kuwa kimya kwenye muziki.

Image result for soggy doggy hunter 
Soggy Doggy

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here