Hakuna asiyejua kwamba ni tamko la Muheshimiwa John Pombe Magufuli rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa serikali inatakiwa kuhamia mkoani Dodoma.
Jumaa Lunduno amemkamata hitmaker wa ngoma ya Moyo Mashine Benpol ambaye ni mzawa wa mkoani Dodoma na kupiga nae story kuhusiana na jambo hilo limekaa vipi, na ananeno gani kwa vijana wenzake wa mkoani Dodoma.
“Waangalie fursa wang’amue, kilimo cha mazao ya chakula kitapanda thamani, uwekezaji, maduka ya vyakula, waziangalie hizo fursa kama ukodishaji magari, cha msingi ni kuangalia wapi unaweza, capital yako inatosha wapi, kama kuna taasisi za mikopo nenda kopa kisha anzisha miradi yako ambayo unajua watu wakija unaweza kupata wateja wengi.”
Na hicho ndicho alichokiseam Benpol, unaweza kumsikiliza hapa chini alivyokuwa akizungumza mwenyewe baada ya kusogezewa kipaza cha Jumaa Lunduno akiwa backstage ya jukwaa la Fiesta Moshi.
No comments:
Post a Comment