Ben Pol:- Mimi ni msanii wa kwanza nchini kuleta muziki wa RnB uwanjani - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 16 November 2016

Ben Pol:- Mimi ni msanii wa kwanza nchini kuleta muziki wa RnB uwanjani

Image result for Ben pol
Mkali wa muziki wa RnB, Ben Pol anaamini kuwa yeye ndio msanii pekee aliyesababisha show za muziki wa RnB kufanyika uwanjani tofauti na zamani zilikuwa zikifanyika ukumbini pekee.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa hapo mwanzo watu walizoea kuwaona wasanii wa RnB wakifanya show ukumbini tu.

''Naweza kusema kuwa mimi ni msanii wa kwanza kulete muziki wa RnB uwanjani, watu walishazoea wasanii wa RnB kufanya show ukumbini tu. Kwa sasa wasanii wa RnB tunaweza kufanya show uwanjani mbele ya mashabiki zaidi ya elfu sitini hadi sabini ni kitu kikubwa. Lakini kama sitakuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo basi nitakuwa ni miongoni mwa wasasnii waliofanya hilo likawezekana.''

Ben Pol ameongeza kuwa atahakikisha anaachia kazi yake mpya siku si nyingi kwa ajili ya kufunga mwaka na kuanza mwaka vizuri.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here