Hii ni habari nzuri kwa mashabiki wa Bongo Flava Ni kuhusiana na kuludi upya kwa kundi la Wakacha linalorudi na nguvu mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na wasanii wanaounda kundi hilo kuwa kuwa busy na kazi zao binafsi.
Rapper Cyrill aka Kamikaze, amevujisha siri hiyo wakati akipigia mstari kupitia kipindi cha THE SPLASH kinachosikika kupitia Ebony FM.
''Jana tulikuwa tuko studio mimi, Jux pamoja Flow, tumeshafanya ngoma ,tunachosubiri ni mipango tu ya video. Kwahiyo Wakacha ipo, Wakacha ni familia, Wakacha ni zaidi ya kundi ni kama familia,''alisema Cyrill.
''Ujue familia kama jina fulani la Familia haliwezi kubadilika miaka ikaenda ikarudi, sawa mtaenda kila mtu na kazi yake lakini jina la familia litabaki. Kwahiyo hata sisi Wakacha tunafanya solo lakini tunajipa time. This time around tumejipanga kuwapa mashabiki ngoma hatujapanga tu tarehe,'' aliongeza.
Katika hatua nyingine, Cyrill amezungumzia sababu za kuchelewa kwa video ya ngoma yake ya Cheza Kidogo.
''Cheza kidogo nilisimamisha project kwa sababu nilishaanza video, lakini baada ya ile mvutano na WCB na menejimenti ya Ray Vanny kuingia pale kati na kusema wimbo ulikuwa hivi na vile, nikaona niisimamishe. Hata sikuisimamia sana kama hata ukigundua sikuweka nguvu kubwa sana kwenye promo maana niliona kama nitaonekana nataka kuiforce hivi,'' alisisitiza Cyrill.
Rapper huyo amesema kuna ngoma mbadala ya Cheza Kidogo anayoamini ni ni kali na inakuja na video baada ya wiki moja au wiki moja na nusu kuanzia sasa.
Cyrill Kamikaze & Jux... Wakacha
No comments:
Post a Comment