Thursday, 17 November 2016

Mr T-Touch aeleza kwanini watayarishaji wa muziki hutoa beat bure kwa wasanii

Image result for Mr T –Touch
Producer Mkali na aliyetengeneza hits kibao, Mr T –Touch amefunguka kwa kuitaja sababu inayowafanya watayarishaji wengi wa muziki kuwapatia beat bure wasanii.

Mtayarishaji huyo amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM,
''Tunatoa beat bure ili tuweze kuaminiwa. Nimetoa beat za bure kwa takribani miaka mitatu.''

Mr T –Touch ameongeza kuwa hakuna producer anayenufaika kupitia studio yake labda awe na kazi nyingine nje ya muziki. Kwa sasa Mr T –Touch anamiliki studio yake inayojulikana kwa jina la Touchez Sound aliyoifungua mwezi Julai mwaka huu.

Image result for Mr T –Touch
Mr T –Touch ndani ya Studio yake Touchez Sound

No comments:

Post a Comment