Kwenye kipindi cha XXL cha Clouds fm ndipo ngoma hiyo ilizinduliwa rasmi na mwanadada Vanessa Mdee akatusanua kuwa kichupa cha ngoma hiyo kitaachiwa rasmi leo katika mitandao ikiwa ni tayari imekwisha wasilishwa katika vituo mbali mbali vya Televisheni ikiwemo Clouds TV. Kama umefuatilia vipindi mbali mbali vya Clouds TV leo hii naamini umekwisha kutana na kuitazama video hiyo.
Point ya msingi ni leo kwenye kipindi cha Clouds E ambapo Mwana FA alikuwepo ili kutusanua vitu ambavyo tulikuwa hatuvifahamu kuhusiana na video hiyo.
Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba video hiyo imefanywa mara mbili na mmoja kati ya madirector wakubwa sana nchini South Africa baada ya version ya kwanza kutowaridhisha wakali hao.
Mwana FA amedai kuwa video ambayo aliletewa mara ya kwanza hakuikubali kutokana na video hiyo kutoendana hata kidogo na idea ya wimbo na hivyo kulazimika kumwambia director huyo kuirudia tena video hiyo.
''Mara ya kwanza ilikuja lakini sisi hatukuwa tumeridhika na viwango ambavyo ilikuwa navyo kulinganisha na vile ambavyo sisi tulikuwa tunavihitaji. Sio viwango vya picha au nini lakini ni tafsiri ambayo sisi tulikuwa tunaipata kutoka kwenye wimbo haikkuwa tafsiri yenye kutosha kuwakilishwa na video ambayo tulikuwa nayo mara ya kwanza, kwahiyo ikabidi nisafiri tena kwaajili ya kushoot video nyingine.'' Alisema Mwana FA
Unaweza ku-download hapa Music Audio Mwana FA ft Vanessa Mdee - Dume Suruali
No comments:
Post a Comment