Msanii mkongwe katika game la bongo fleva Q Chilla amesema hajawahi kumpigia simu msanii yoyote hapa Tanzania kumuomba wafanye kolabo japo yeye amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali wakimuomba kufanya naye kolabo.
Akiongea ndani ya eNewz Q Chilla amesema huwa ana angalia muda wake pale anapo pigiwa simu za kuombwa kolabo na mara nyingi ana angalia malipo na muda.
Q Chilla pia alisema aliamua kuchukua maoni ya watu walipo mshauri kuwa akitaka kupiga kolabo afanye na Diamond kwa kipindi hiki, ndiyo akaamua kuufanyia kazi ushauri wa mashabiki zake.
Mbali na hayo pia Q Chilla hakusita kumsifia Alikiba kuwa ana stahili kuwa KING na anapenda ngoma zake ila kuna utofauti kati yao hivyo watakapo kutana kwenye kolabo ni lazima wafanye wimbo wa tofauti sana kwa kuwa wote ni wakali wa voko.
Q Chilla
No comments:
Post a Comment