Raymond atuhumiwa kuiba baadhi ya mistari kwenye wimbo wa msanii wa Singeli - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 17 November 2016

Raymond atuhumiwa kuiba baadhi ya mistari kwenye wimbo wa msanii wa Singeli

Image result for Manyo Lee na raymond
Msanii Mkali wa kutafuta Kiki kutoka WCB, Raymond {Rayvanny} anatuhumiwa kutumia baadhi ya mistari ya wimbo wa msanii wa muziki wa Singeli, Manyo Lee kwenye ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ''Sugu''.

Msanii huyo wa Singeli, Manyo Lee Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio,  alisema..

''Mimi nilisikia kwa watu tu kuwa dogo kachukuwa mashairi yangu. Juzi kati lilifanyika tamasha kubwa tu nikaona akiimba yale mashairi lakini nikaona kawaida tu lakini hivi karibuni nimeona kaachia video kabisa nikaona kumbe dogo yupo serious kabisa.''

''Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu funga virago shetani. Joh Makini akiwa mweusi Barakah tumuite nani?,'' huo ndio mstari ambao Manyo Lee anadai Raymond {Rayvanny} kauchukua kwenye wimbo wake unaoitwa 'Mwendo wa Pushapu'.

Nae Manyo Lee katika wimbo wake aliouachia mwezi Septemba mwaka huu ameimba, ''Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu virago funga shetani. Makini ajiite mweusi na Nigga ajiite nani?.''

Download Hapa Music Audio Manyo Lee - Mwendo Wa Pushap...

Image result for Manyo Lee - Mwendo wa Pushap

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here