Instagram na mitandao mingine ya kijamii kama Youtube, Facebook na Snapchat ni mizuri sana ikitumika kwa malengo kwani inasaidia mambo mengi sana, na hii wote tunajua kama sio kuona mitandao hii ikitoa ma-super star lukuki kwa kuonesha vipaji vyao kupitia huko.
Ijumaa ya wiki iliyopita kulikuwa na Toronto Raptors game ambapo mchezo huo ulihudhuriwa na Drake huko alikutana na Mtoto wa miaka saba aliye tambulika kwa jina la Young Dylan ambae ni moto wa kuotea mbali pale unapompa kipaza sauti.
Huyu dogo stori yake ni kwamba kazaliwa miaka 7 iliyopita Jijini Toronto nchini Marekani.
Umaarufu wa Young Dylan hata hivyo ulianzia Kwenye mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa Instagram wa mama yake kabla ya kufunguliwa Akaunti yake ambayo anaitumia hadi sasa.
Young Dylan alikuwa akirekodiwa na mama yake akiimba nyimbo za Drake karibia zote, na ndipo ule mchezo wa kutag ukaanza mpaka Drake akapata video za Dogo akiimba nyimbo zake tena kwa ubora uliotukuka.
Sasa Dogo Young Dylan alipata muda wa kuperfom kwenye muda wa mapumziko wa Mechi hiyo ndipo akaanza kwa kuimba wimbo wa Drake wa For Free.
Unaweza kumcheki kwa kutazama video yake hapa....
No comments:
Post a Comment