Msanii wa zamani wa muziki wa asili Saida Karoli amedai yeye anasikia kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond ameiangia mkataba na meneja wake wa zamani kuhusu kutumia vionjo vya nyimbo zake katika kutengeneza wimbo Salome wa Diamond.
Saida Karoli
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo Salome ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.
''Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,'' alisema Saida Karoli katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. ''Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,''
Pia muimbaji huyo amedai kuwa yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.
Diamond na uongozi wake baada ya kuachia wimbo huo, walionyesha picha wakati wakifanya makubaliano na meneja wa zamani wa Saida Karoli.
''Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,'' Diamond alikiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.
Tazama hapa video ya mazungumzo ya Saida Karoli katika runinga ya KUTV
No comments:
Post a Comment