P the Mc ameongea haya kufuatia release ya ngoma ya Bagdad na Roma ft Snura “K ni K”, P the Mc anasema
''mabadiliko waliyo yafanya kimuziki ni mazuri kwa fikra za kujipatia mashabiki tofauti lakini sina uhakika kama wale mashabiki wao wa mwanzo watapenda au la, unaweza ukaongeza mashabiki 8 alafu ukapunguza 10, nikiwa kama msanii nasema sio mabadiliko chanya”
P the Mc ambaye anatarajia kuachia refix ya All the way up ijumaa hii anasema Bagdad na Roma waliwahi kufanya ngoma ya pamoja “Una Akili Wewe” ikafanya vizuri na mashabiki wakaipokea vizuri
“ waliweza kufanya wimbo wa una akili wewe katika maadhi yao ya kila siku na ikawa poa tu, sio lazima kuhama misingi”
Ngoma mpya ya P the Mc All the way up Refix itakua exclusive hapa hapa siku ya ijumaa so stay tune.
No comments:
Post a Comment