Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amesema ameachia wimbo ‘Furaha’ ili kumfariji msanii wenzake Dogo Janja aliyefiwa na Baba yake hivi karibuni.
Rapa huyo ambaye alikuwa kimya kwenye muziki tangu atangaze kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai hakuwa na mpango wa kuachia wimbo huo kwa sasa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Dee ameandika:
''Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana. Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo imara sana katika maisha yake. Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia wimbo wangu wiki hii. Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I have Nothing But Love to You''.
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection Dogo Janja alifiwa na baba yake mzazi siku ya Jumapili, Abubakari Chande.
Mzazi wake huyo ambaye alikuwa akiishi mkoani Arusha, ni mmoja kati ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wanamshauri katika muziki wake.
Kupitia mtandao wa Instagram, tuliweza kupata taarifa hiyo kutoka kwenye ujumbe aliouandika.
"PUMZIKA KWA AMANI BABA YANGU KIPENZI.😠Hakika MUNGU Amefanya Maamuzi Yake Siwezi Kukufuru Zaidi Ya Kukuombea kwa ALLAH akupe kauli Thebeet! Umelala baba yangu sitakuona tena😠EEH MWENYEZI MUNGU UMPOKEE,UMUONDOLEE ADHABU ZA KABURI. Lala baba hakika wote njia yetu ni moja.. siku moja tutaonana tena baba! R.I.P Kamanda ABUBAKARI CHENDE!''
No comments:
Post a Comment