Young Dee {Paka Rapa} kwa mara ya kwanza amuona mwanae..... - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 12 December 2016

Young Dee {Paka Rapa} kwa mara ya kwanza amuona mwanae.....

Damu ni nzito kuliko maji, hata kama utakataa usoni lakini nafsi yako na moyo vitazungumza ukweli na utabaiki hivyo daima.


Jambo la busara zaidi ambalo Young Dee amewahi kufanya katika maisha yake basi hili ni jambo la kipee zaidi, kwa kumkubali mtoto na kuchukua majukumu kama baba. Jambo ambalo vijana wengi hushidwa kulifanya.

Chek hapa chini  baadhi ya post alizoziweka Young dee kwenye ukurasa wake wa Istagram.

A photo posted by PAK👁RAPPER (@youngdaresalama) on


Nawashukuru sana watu wote ambao wamekuwa waki-support kazi yangu mpya #Furaha Either Naomba radhi kwa mashabiki zangu ambao wamekwazika kwa njia moja au nyingine kutokana na taarifa za uongo zilizosambaa mtandaoni. Ikumbukwe tarehe 22 June mwaka huu niliitisha press nikaomba radhi kwa waTanzania na mashabiki zangu wote kwa ujumla, nikaeleza kuwa nimepitia kipindi kigumu sana na kuwa kuna mengi nimefanya ambayo sijivunii na najutia. Niliahidi kubadilika na kuwa mfano mzuri kwa jamii. Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikipigana na nafsi yangu kuhakikisha sirudii makosa. Madhara yanayotokana na matendo niliyofanya kipindi kile hadi leo bado yananitafuna ila nimekuwa nikijitahidi kukabiliana nayo. Nilipewa taarifa na mamisa kuwa ana mimba yangu ya (miezi 6), kama kijana nilishtuka na kupata ugumu kuikubali hali hiyo kutokana na kwamba nilikua nimetoka kwenye kipindi kigumu. Baada ya kutafakari nilimuomba aitunze hiyo mimba asiitoe!!! Kama ni mwanangu ntamlea. Kama ningekuwa na nia ya kumkana mtoto au kumtelekeza, kwanini nimwambie asitoe? Si kutaka kumshirikisha mtu kwanza bila kuwa na uhakika kwamba kweli mtoto ni wangu. Management yangu sikuishirikisha kwa lolote kwa sababu inanisaidia sana katika kuhakikisha career yangu ya music ina imarika. Hivyo nilihisi ni taarifa ambayo inaweza kui-disappoint na kukatisha malengo. Hata familia yangu Mama, dada na ndugu sikuwaeleza kitu. Nilitaka nijipange vizuri, nijihakikishie kweli mtoto ni wangu, nitafute njia sahihi ya kueleza hili jambo. Nimesikitika sana kuona kuwa sio kila mtu anafurahia unapofanikiwa, unapoamua kufanya kazi ili upate maendeleo. Wapo watu ambao bado watatafuta fursa ya kukuharibia maisha. Yote kheri Namuachia mungu baba. Mtoto wangu nimempokea kwa moyo mmoja. Ni mtoto wa kike, na anaitwa Tamar. Nimewataarifu ndugu na wazazi wangu kuhusu hili, nashukuru wamenielewa. Nimeuelewesha pia uongozi wangu, wamenielewa. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa Kumjaalia uhai mwanangu, amezaliwa akiwa salama kiafya. Shukrani za dhati ziende kwa uongozi wangu, kwani wamekua wakihakikisha nasimama katika njia sahihi bila kuyumba. Shukrani kwenu SHILAWADU kwa kujaribu kuzirudisha nyuma jitihada zangu za kimaendeleo. #YoungDaddy
A photo posted by PAK👁RAPPER (@youngdaresalama) on



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here