Young Dee:- Situmii Dawa za Kutunisha Misuli - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 5 December 2016

Young Dee:- Situmii Dawa za Kutunisha Misuli

 Image result for young dee 2016
Mkali wa hip hop nchini Paka Rapa Young Dee amesema hatumii dawa zozote za kukuza misuli yake na mwili wake bali anafanya mazoezi kila siku na bado hajafikia katika kiwango ambacho anataka kufikia.

Hata hivyo akiongea kupitia eNewz, Young Dee amesema anazingatia chakula, muda  wa mazoezi na muda wa kupumzika na pia anazingatia sana chakula  chenye protini na mahali pazuri pa kulala, hizo ndizo sababu ambazo zinampelekea kuwa na mwili mkubwa kwa sasa.

Pia Yong Dee amemalizia kwa kusema kwamba hajawahi kuachana na mpenzi wake Tunda hivyo hata sasa Tunda anavyomposti katika mitandao yake na kumshukuru Young Dee ni kutokana na ushauri ambao alimpa hivi karibuni kuhusiana na maisha yake

 Related image 
                           Young Dee {Paka Rapa} & Tunda

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here