AT Ameamua Kumtolea Povu Rama Dee kuhusu Kudiss Director Adam Juma..... - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 21 March 2017

AT Ameamua Kumtolea Povu Rama Dee kuhusu Kudiss Director Adam Juma.....


Mwanamuziki wa miondoko ya miduara nchini Tanzania AT ambaye ni Mfalme wa miduara na kwa sasa anatamba na ngoma mpya yenye mahadhi tofauti na mduara inayokwenda kwa jina la Sili feel, ameamua kumchana msanii Rama Dee kwa kumwambia anapaswa awaheshimu watu waliomtangulia kiuwezo.

Hayo yamekuja siku chache baada ya msanii Rama Dee kusema kiwango cha Director Mkongwe ncini Tanzania Adam Juma wa ''Next Level'' kiko chini ya viwango katika kutayarisha na kutengeneza video na kwamba anamtaka ajifunze kutoka kwa Hanscana.
''Imekuwa desturi kwenye nchi yetu mtu kutomuheshimu mwenzake au nguvu zake, leo unatoka unasema Adam Juma hajui ku-shoot ‘video’, wakati wewe ukipewa ile kamera hata kupiga picha huwezi kujua lakini yule mtu ndiyo amekuja muziki wa Tanzania''. Alisema AT kwenye eNewz.
 Image result for Director adam juma
Siku za nyuma Jambo hilo lilipelekea Adam kunukuliwa akisema
“Mimi nimepumzika na sitaki kufuatilia mambo hayo ya muziki kila mtu ana misimamo yake na kwa sasa nataka niache kabisa mambo ya muziki nataka nifanye mambo yangu mengine ni ‘relax’ na kama kuna mtu anahisi mimi ni mjinga au mpumbavu ‘it’s fine.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa Director Adam Juma kutangaza kuachana kufanya video Aliwahi kusema hivyo miaka miwili iliyopita, lakini akatengua kauli yake kimya kimya na kuanza kufanya tena kwa jina la AJ.

Aidha AT amesema wasanii ndiyo wanaongoza kwa kutokuwa na heshima, hivyo amewataka wasanii wenzake kuwa na heshima kwa watu waliowazidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here